Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam imeamua kuwasomesha wanafunzi wa kidato cha nne watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano na sita.

Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda  ameeleza kuhusu uamuzi huo wakati akipokea msaada wa madawati 200 yenye thamani ya Sh milioni 20 kutoka kwa shule za Almuntazir jijini humo.

Amesema ofisi yake imeona ni vyema kuanza kwa kuwasomesha wanafunzi hao ili kuongeza idadi ya wataalamu wa sayansi katika sekta mbalimbali nchini.

Amesema pia walimu waliowafundisha wanafunzi hao watapewa fedha taslimu Sh milioni mbili kila mmoja na kupelekwa kutalii katika mbuga za wanyama na mke au mume wa mwalimu husika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Khoja Shia Ithna Asheri Jamaa (KSIJ), Imtiaz Lalji, inayomiliki shule hizo amesema wanampongeza Rais John Magufuli kwa juhudi zake za kukuza sekta ya elimu nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *