Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa wanafunzi wa Lucky Vicent wanaotibiwa nchini Marekani wanatarajiwa kurejea nchini mwezi wa Agosti mwaka huu.

Watoto hao watatu walinusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya mjini Arusha.

Nyarandu ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa  mtandao wa kijamii wa Facebook na kueleza kuwa wanafunzi hao kwasasa wanaendelea vizuri.

Pia Nyalandu amesema kuwa watoto hao ambao ni Doreen Mshanga, Saidia Ismael na Wilson Tarimo wanategemewa kutembea tena.

Hata hivyo, kwa sasa Doreen atahamishiwa katika kituo maalumu kwa ajili ya matibabu ya uti wa mgongo cha Madonna katika mji wa Lincoln, Nebraska.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *