Wanadiplomasia 35 wa Urusi waliofukuzwa na rais Barack Obama kutoka nchini Marekani wameondoka wakiandamana na familia zao.

Urusi ilituma ndege maalum ya kuwarudisha nyumbani wanadiplomasia hao ambao wanahusishwa na udukuzi wa uchaguzi wa Marekani ulifanyika mwaka jana na Donald Trump kushinda kiti cha urais.

Wanadiplomasia hao waliamuriwa kuondoka Marekani baada ya Urusi kushtumiwa kuwa ilijaribu kuingilia uchaguzi wa hivi majuzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.

Vyombo vya kijasusi vya Marekani vinadai kuwa utawala wa Urusi ndio ulioamuru kudukuliwa kwa hasa tovuti ya chama cha Democratic ili kuvuruga kapeni za bi Clinton na kumsaidia Donald Trump ambae sasa ndiye rais mteule wa taifa hiyo.

Kwa upande mwingine Donald Trump alimpingeza rais wa Urusi Vladimr Putin baada ya kutolipiza kisasi cha kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani waliopo nchini Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *