Rais wa Marekani, Barrack Obama ameamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa thelathini na tano wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo nchini Marekani.
Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.
Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa upande wake, rais mteule wa Marekani, Donald amezipuuzilia mbali taarifa hizo za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa Marekani ili kulijadili hilo.
Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.