Mamlaka ya Idara ya leseni Zanzibar imesema itawachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafutia leseni zao wamiliki wa magari ya abiria watakaobainika kujishughulisha na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Leseni Suleiman Kirobo wakati alipozungumza na wamiliki wa magari ya abiria yanayotoa huduma za usafiri kwa abiria wa Unguja.

Amesema yapo malalamiko mengi yanatolewa na jamii kuhusu kuwepo kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyofanywa na makondakta wa gari za abiria dhidi ya wanafunzi.

Kirobo amesema baadhi ya njia za magari ya abiria zinazotoa huduma ambazo zinazohusika na vitendo hivyo vya udhalilishaji kijinsia abiria ni daladala za Fuoni, Mwanakwerekwe na kwamba makondakta wake pia wanatuhumiwa kutoa lugha chafu kwa abiria.

Mmoja ya wamiliki wa gari zinazotoa huduma katika barabara ya Fuoni alisema wameyapokea malalamiko hayo na wao watayafanyia kazi kwa lengo la kuondoa kero hiyo kwa abiria ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *