Wafanyabiashara wadogo ‘Wamachinga’ jijini Mwanza wamemshukuru rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli baada ya kuwaruhusu kufanya biashara katikati ya jiji hilo.

Wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela walihamrisha wamachinga waondoke katikati ya jiji la Mwanza agizo ambalo limekataliwa na rais Magufuli.

Baada ya tangazo hilo kutolewa machinga hao walilipuka kwa shangwe na bila kuchelewa walianza kurudisha biashara katika maeneo yao huku mgambo wakibaki wameduwaa.

Aidha machinga hao wamesema wanamshukuru Rais kwa kuingilia kati mgogoro huo kwakuwa maeneo waliyokuwa wamepelekwa hayakuwa rafiki kwa biashara zao kutokana na umbali.

Mwenyekiti wa Machinga jijini Mwanza Said Tembo amesema wanamshukuru sana Rais na hawana cha kumlipa na kusema kuwa ndani ya siku nne wamepitia mateso makubwa sana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *