Aliyekuwa mshindi wa BSS 2012, Walter Chilambo amesema kuwasasa ameacha kufanya muziki wa Bongo fleva na badala yake ameamia kwenye muziki wa gospel.

Chilambo amesema ameamua kuamia upande wa muziki wa gospel ili kufanya kile anachokipenda zaidi uhenda uko ndio kuna mafanikio yake.

Walter amesema kuwa “Kwa sasa mimi nitakuwa namuimbia Mungu, hata wimbo wangu mpya ‘Asante’ namuimbia Mungu, ni wimbo wa gospel na nimeamua kumshukuru mwenyezi mungu kwa sababu tunapitia mambo mengi sana sisi kama vijana.

Aliongeza kwa kusema ‘Kwa hiyo nimekaa na familia na mimi mwenyewe nikaona nifanye kitu ambacho moyo wangu utakuwa unafurahia pia naimani hata jamii nayo itakuwa rahisi kunisupport kwahiyo najaribu huku labda Mungu ana mpango na mimi’.

Walter Chilambo alipata umaarufu kwenye shindano la BSS baada ya kuimba nyimbo za Ben Pol pamoja na Diamond mpaka kupelekea kuwa mshindi wa BSS mwaka 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *