Wanajeshi maalum wa Uturuki wamewatia mbaroni wanajeshi wanaoshukiwa kufanya jaribio la kumteka rais Recep Tayyip Erdogan wakati jaribio la mapinduzi lililotibuka, lilipoanza wiki mbili zilizopita nchini humo.

PINGU

Takriban makomando 11 wametiwa mbaroni nje ya mgahawa wa Marmaris ambapo rais Erdogan alikuwa ameenda likizoni, japo alitoweka baada ya kudokezewa kuhusu mpango huo kabla ya makomando hao kumvamia na kukamatwa.

Maafisa wamesema ndege zisizokuwa na rubani na helikopta zilitumiwa kuwasaka waharifu hao baada ya kuonekana na wanakijiji wakiwinda ngiri katika eneo hilo la misitu nchini Uturuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *