Waliomuibia Kim Kardashian wakamatwa jijini Paris

0
260

Polisi nchini Ufaransa wamewakamata watu 16 kwa kuhusika na wizi wa kutumia nguvu waliomfanyia mwanamitindo Kim Kardashian mjini Paris mwezi Oktoba mwaka jana.

Kim Kardashian aliporwa kwa nguvu na takriban watu wawili waliokuwa wamevaa sare za polisi katika jiji la Paris nchini Ufaransa.

Watu waliomuibia staa huyo waliingia chumba cha kifahari alichokuwa Kim Kardashiana kabla ya kumfunga na kumfungia kweye bafu.

Polisi wa Ufaransa wamesema kuwa uchunguzi wa DNA ndio ulichangia kukamatwa kwa watu hao.

Watu hao waliokamatwa wakati wa uvamizi ulioendeshwa maeneo ya Paris, Normandy na la Frech Riviera kufutia uchunguzi wa miezi kadha.

Moja ya uchunguzi wa DNA ulikuwa sawa na ule wa mtu anayejulikana kwa polisi kuwa mhalifu.

Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki Kanye West amesema alikuwa na hofu kuwa angeuawa wakati huo kipindi alipokuwa jijini Paris kwa ajili ya maonesho.

Kardashian mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 36 alikuwa mjini Paris kwa maonyesho ya mitindo.

 

LEAVE A REPLY