Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amewaagiza wote waliohitimu kidato cha sita Mei mwaka huu na ambao hawajajiunga na vyuo vya elimu ya juu wakaripoti katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Disemba Mosi, mwaka huu.

Dk Mwinyi amesema Mei na Juni mwaka huu, JKT iliwafanyia usaili vijana wa kujiunga na JKT kwa kujitolea.

Amesema usaili huo ulifanyika kwa kushirikiana na kamati za ulinzi za wilaya na mikoa.

Dk Mwinyi amesema mafunzo hayo ni ya miezi mitatu kwa mafunzo yenye utaratibu wa kawaida na miaka miwili kwa wa kujitolea.

Ili kufanikisha hilo, Wizara ilimuagiza Mkuu wa JKT kufufua kambi ya Makuyuni JKT iwe miongoni mwa kambi kuanzia Desemba mwaka huu.

Ameagiza kambi za Luwa na Milundikwa za mkoani Rukwa, zirejeshwe kwa shughuli za JKT za kilimo na ufugaji.

Dk Mwinyi alimuagiza Mkuu huyo wa JKT pia kambi ya Mpwapwa irejeshwe kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya kilimo na ufugaji ndani ya JKT.

Juni mwaka huu, vijana 14,000 waliohitimu kidato cha sita mwaka huu, walijiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.

Vijana hao walimaliza mkataba wa miezi mitatu mwanzoni mwa Septemba, mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *