Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga miili ya waliokufa kwenye tetemeko la ardhi mjini Bukoba mkoani Kagera.

Wananchi kwa makundi wanaelekea katika uwanja wa Kaitaba ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amesema kuwa Waziri mkuu, Majaliwa ataungana na waombolezaji na kuzungumza na wananchi kuhusu tukio hilo la jana lililosababisha vifo na majeruhi.

Hadi usiku wa kuamkia leo vifo vilikuwa vimefikia 14 na majeruhi zaidi ya 200 ambao wanahudumiwa katika maeneo mbalimbali.

Tetemeko hilo lenye ukubwa (magnitude) wa 5.7 limetokea jana katika mikoa ya Mwanza, Kagera na sehemu za Shinyanga.

Tetemeko hilo la ardhi limetokea mida ya saa kumi jioni siku ya jana na kusababisha watu kushikwa na taharuki juu ya tukio hilo ambalo ni geni hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *