Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya darasa la saba huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 2.52 lakini kumetokea na udanganyifu kwa baadhi ya shule.

Baadhi ya waliohusika na udanganyifu huo ni walimu, wamiliki wa shule na wasimamizi wa mitihani ambao walikuwa wanawatajia majibu wanafunzi pamoja na kuwaandikia wanafunzi hao majibu kwenye sare za shule.

Wakati wa ushaishaji wa mitihani hiyo baadhi ya shule ziligundulika kutokana na wanafunzi kufanana majibu ya kupata na kukosa kitu ambacho si kawaida kutokea kwenye mitihani huku udanganyifu mwingine ulikuwa kwa mwalimu mkuu kuandaa majibu na kumpa msimamizi.

Vile vile baadhi ya walimu walikuwa wakiwafanyia mitihani wanafunzi wao lakini walikamatwa na maafisa wa TAKUKURU na kamati ya elimu za mikoa yao.

Maelezo hayo yametolewa na Katibu mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonde wakati akitangaza matokeo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Shule zilizohusika na udanganyifu huo ni

  1. Shule ya msingi Tumaini iliyopo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza

2. Little Flower iliyopo Sengerema mkoani Mara

3. Mihamakumi iliyopo iyopo wilani Sikonge mkoani Tabora

4. Qash iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara

5.St Getrude iliyopo Madaba mkoani Ruvuma

6. Kondi, Kasandalala iliyopo wilayani Sikonge mkoano Tabora

barua

barua2

barua3

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *