Wakulima wa kahawa mkoani Kilimanjaro wameshindwa kunufaika na zao hilo kutokana na kujihusisha zaidi na uzalishaji na kushindwa kusindika ili kuiongeza thamani na kuingia kwenye ushindani wa soko la kitaifa na kimataifa.

Zao hilo, ambalo katika Mkoa wa Kilimanjaro linaonekana kulimwa zaidi na wanawake, halijaonyesha mafanikio makubwa ya maendeleo kwa wakulima hao, jambo ambalo linaelezwa kuchangiwa na wengi wao kujikita kwenye uzalishaji na wengine kulima kwa mazoea.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Tanzania Women in Coffee Association (Tawoca), Fatma Faraji, wakati wa kujifunza namna ya kutengeneza kahawa kupitia mashine ya expesso ili kuiongeza thamani.

Pia amesema kuwa ili wakulima waondokane na dhana hiyo ya kulima kahawa pasipo kuziongezea thamani, ni vema wakulima wapewe elimu ya usindikaji bora wa kahawa ili kilimo hicho kiweze kuwanufaisha kiuchumi.

Ameongeza kwa kusema kadri wanawake watakapoelimishwa kuhusiana na mnyororo wa thamani, usindikaji na masoko, zao hilo ambalo limedorora katika mkoa huo litakua kwa kasi tofauti na ilivyo sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *