Wakulima wa vitunguu wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamelalamikia baadhi ya kampuni zinazozalisha mbegu za zao hilo kwa kuwauzia mbegu feki na kusababisha kuzalisha mazao yaliyo chini ya kiwango na hivyo kukosa soko.

Wakulima hao wamesema mbali na uzalishaji wa vitunguu kushuka, kitendo hicho kimewaondolea uaminifu kwa baadhi ya kampuni.

Mmoja wa wakulima hao, Raphaely Mbendo, alisema: β€œKuna paketi za mbegu za vitunguu kutoka kwa baadhi ya kampuni zinaonyesha picha ya vitunguu vyekundu ambavyo soko lake linapatikana mahali popote ndani na nje ya nchi lakini vinapopandwa vinatoa rangi nyeupe tofauti na matarajio yetu,” alisema Mbendo.

Naye mjumbe wa Bodi ya Ushirika wa wakulima wa vitunguu katika skimu hiyo, Pascal Zawadi, aliwataka viongozi wa kampuni za uzalishaji wa mbegu za vitunguu nchini kuwatembelea mawakala wa uuzaji wa mbegu hizo na kuzikagua ili kubaini watu wanaozichakachua kwa manufaa yao.

Pia Β Zawadi amesema endapo ukaguzi utafanyika kila mara wale wanaowahujumu wakulima kwa kuwauzia mbegu feki zisizo na ubora watabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *