Wananchi wa vijiji vya Kiwege na Mlilingwa wilayani Morogoro wameomba kurejeshewa zaidi ya ekari 20,000 walizozitoa kwa wawekezaji ambao wameshinda kuziendeleza.

Wakazi wa vijiji hivyo wamemuomba waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kubatilisha milki ya ardhi hiyo ili irejeshwe kwa wananchi.

Wakizungumza na wataalamu kutoka Mtandao wa Jamii wa Uhifadhi ya Misitu Tanzania (MJUMITA)  wananchi hao wamesema kuna mashamba mengi yametolewa kwa wawekezaji wakiwemo wafugaji lakini wameshindwa kuyaendeleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *