Wakazi wa mkoani Dar es Salaam wanatarajiwa kumeza kinga tiba ya mabusha, matende na minyoo kwa siku tano kuanzia Oktoba 25 mwaka huu.

Mratibu wa kitaifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs), Dk Upendo Mwingira amesema watu wote wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea watatakiwa kumeza dawa hizo.

Mwingira amesema dawa hizo hazina madhara yeyote kwa binadamu kama ambavyo mara kwa mara imekuwa ikidaiwa hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumeza dawa hizo ili kujikinga dhidi ya magonjwa hayo ya mabusha, matende na minyoo ambayo huathiri ini na ubongo.

Amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda atakazindua umezaji dawa huo katika kituo cha afya Buguruni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *