Staa wa miundoko ya Hip-Hop nchini, Wakazi anatarajia kuachia albam yake mpya inayokwenda kwa jina la “Kisimani” ambapo amewashirikisha wasanii tofauti kwenye albam hiyo.

Wakazi amesema kwamba albam hiyo ambayo ameifanya na watayarishaji tofauti nchini inakaribia kukamilika kwa hiyo mashaki wake wakae mkao wa kula kwa ajiri ya kuipokea albam hiyo mpya.

Staa huyo amabaye ameamua kutoa albam kwasasa baada ya kuzoea kutoa mixtape hapo awali, amesema itakuwa ni hatua kubwa kwa yeye kutoa albam hiyo ingawa soko siyo zuri lakini anaweza kuisambaza kwa njia ya mtandao.

Staa huyo aliwahi kutamba na nyimbo kama Natokea Dar, Kanuni za hela na Tayari kwa yote ni miungoni mwa nyimbo zilizomtambulisha katika ulimwengu wa mzuiki wa Hip-Hop.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *