Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Wakazi amezidi kumchana Godzilla kwa kumwambia asijisumbue kwa madai ana kazi nyingi za ‘mix stape’ ambazo anaweza kuzitumia wakati huu wa ugomvi wao.

Wakazi amebainisha hayo ikiwa ni siku moja kupita tokea apate kura nyingi zilizopigwa na wananchi kwa kumchagua msanii wanaomkubali baina ya hao wawili.

Wakazi ambaye ni memba wa kundi la SSK amesema kuwa “Godzilla mimi haniwezi kwenye kuandika hata free style ila mimi ninampa tu heshima yake ya ku-free style kama ninavyompa Nikki Mbishi. Ana mapungufu mengi tu kuyaelezea lakini kama ametaka tumeamua kuyaelezea ila tu asijisumbue na ‘body of work’ nina kazi nyingi ‘mix stape’ sita, albamu tunatafuta tu mazingira ya kuzitoa ‘maybe’ mazingira yenyewe ndiyo haya sasa “.

Pamoja na hayo, Wakazi amesema si kweli kwamba anamuonea Godzilla kwa kuwa ametambua ana msongo wa mawazo kwani hata yeye mwenyewe pia anatatizo hilo pia linalomsibu kwa upande wake hivyo amemtaka aache visingizio visivyokuwa na nguvu.

Mwisho amesema kuwa “Mimi sijui Godzilla anapitia vitu gani sasa hivi lakini mimi mwenyewe nina msongo wa mawazo nina binamu yangu amelazwa Muhimbili anahitaji figo na mpaka sasa sijui nafanyaje ‘so’ hakuna asiyekuwa na mawazo, kwenye muziki huwezi kusema kwamba hiki ndiyo kipimo cha mafanikio au ndiyo kipimo cha mtu huyu anaweza au hawezi kwa sababu kama hivyo yeye ndiyo anasemekana ndiyo ‘the best in free style’ halafu sasa inakuaje naaambiwa namuonea au ndiyo inawezekana alishinda wakati mimi sikuwepo?”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *