Wajumbe wa Jopo la Kumchagua Rais nchini Marekani wataanza utaratibu wa kuthibitisha matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo kuanzia leo.

Katika uchaguzi wa awali mshindi wa kura nyingi kawaida alikuwa ndiye anapata kura nyingi za wajumbe na hatua ya kumuidhinisha ilikuwa tu ya kutimiza wajibu.

Rais mteule Donald Trump wa chama cha Republican alishinda kwa kupata kura nyingi za wajumbe kutoka kwa majimbo yaliyokuwa yanashindaniwa.

Mpinzani Hillary Clinton, ambaye alikubali kushindwa, alipata kura nyingi za kawaida, ambapo alimzidi Bw Trump kwa zaidi ya kura milioni mbili nusu kote nchini humo.

Hilo limezua mjadala mpya kuhusu mchango wa Jopo la Kumchagua Rais ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Electoral College nchini Marekani.

Watu karibu milioni tano wametia saini ombi la kuwataka wajumbe kuenda kinyume na utamaduni na kumpigia kura Bi Clinton.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *