Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amewataja wasanii watano amabao anawakubali zaidi kwenye Industry ya muziki nchini kutokana na kazi zao na uwezo wao.

Wasanii hao waliotajwa na Lady Jay Dee kutokana na kazi zao na uimbaji wao ni Ben Pol, Ruby, Vanessa Mdee, Shaa pamoja na Mr. Blue ambao wamegusa nyoyo za Jide.

Mwanamuziki huyo ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uimbaji wake wa uimbaji amesema wasanii hao ni miongoni mwa wasanii ambao anawakubali sana kutokana na uwezo wao.

Jide ni miongoni mwa wasanii wakongwe walioanza muziki kitambo lakini hadi sasa hivi anaendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.

Pia Lady Jaydee amesema kuwa soko la albam kwa sasa limekufa lakini hiyo haitamzuia yeye kutoa albam yake na kwamba anatoa albam ili kulinda heshima yake na kuweka heshima kwa mashabiki ambao wanapenda muziki wake.

Lady Jay Dee anatarajia kuachia albam mpya inayokwenda kwa jina la ‘Woman’ mwezi machi mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *