Jarida la maarufu la Forbes linalojulikana kwa kufanya uchunguzi wa kipato cha watu mbalimbali duniani limewataja Wafanyabiashara watano kuwa ndio watu matajiri zaidi Tanzania.

Ifuatayo ni Listi ya Watu Matajiri Tanzania

5. Ally Mufuruki (US$ 110 million)

Ally Mufuruki ni mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya Infotech Investment Limited. Pia ni mwenyekiti wa bodi mbalimbali kama Misingi Limited (Kenya), Legacy Capital Partners Limited (Tanzania), Vodacom Tanzania Limited (Tanzania), Trademark East Africa (Kenya), Chai Bora (Tanzania). Pia ni Mkurugenzi wa bodi ya Blue town Limited (Sweden) na AMSCO (Netherlands)

4.Reginald Mengi (US$ 550 million)

Reginald Mengi ni Mkurugenzi wa Kampuni ya IPP Media inayomiliki magazeti 11, stesheni za redio  10, stesheni za televisheni 3. Anamiliki migodi, Vibali vya Uchimbaji wa madini na coca cola bottling plant pia na viwanda vya kutengeneza bidhaa kama sabuni, maji n.k.

3. Said Bakhresa (US$ 575 million)

Bakhresa ni Mfanyabiashara maarufu ni mvumbuzi na mwenyekiti wa kampuni ya Bakhresa Group of Companies ambayo anahusika na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

2. Rostam Aziz (US$ 1 billion)

Rostam Aziz ni mwanasiasa na mfanyabiashara 2013 Forbes walimtaja kama Mtanzania wa kwanza kuwa bilionea, mwaka 2014 aliuza 17.4% za hisa zake kutoka mtandao wa Vodacom pia anamiliki migodi mbalimbali na vibali vya kuchimba madini.

1.Mohamed Dewji (US$ 139 Billion)

mohammed-dewji

 

Mohammed Dewji ni bilionea mwenye umri mdogo Africa, Ni mkurugenzi wa Kampuni ya METL Group ambayo ni kampuni kubwa, dewji anamiliki asilimia 74  ya kampuni hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *