Mastaa wa Bongo movie, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ wamempongeza waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh Nape Nnauye kutokana na hatua yake ya kudhibiti maharamia wa kazi za sanaa nchini.

Waigizaji hao wamempongeza Waziri huyo kwa harakati zake za kupambana na maharamia wa kazi za sanaa nchini huku wakiwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kwa kununua kazi halali na kuepeuka kununua kazi feki ili kukuza sanaa.

Vile vile waigizaji hao wamesema hapo awali hakukuwa na wizi wa kazi za wasanii kwenye mikanda ya VHS kulinganisha na sasa ambapo wizi huo umekithiri na kusababisha maisha magumu miongoni mwa wasanii.

Wiki iliyopita Waziri, Nape Nnauye alifanya ziara ya kushtukiza kwenye maduka tofauti maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na kubaini kuwepo kwa kiwanda feki kinachotengeneza na kusambaza kazi za wasanii nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *