Serikali imewataka waganga wa tiba asili nchini kuhakikisha wanapata vibali kutoka Baraza la Tiba Asilia kabla ya kupeleka matangazo yao katika vyombo vya habari.

 

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika jana.

 

Bw. John amesema kila mganga wa tiba hiyo anatakiwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na taratibu na kuachana na matangazo yasiyofaa na kuweka mabango ya ovyo barabarani.

 

Aliongeza kwa kuwataka waganga wa tiba asili kujiepusha na migongano katika jamii kwa kuhusisha ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa na kutoa elimu kwa umma kuhusu mkanganyiko huo.

 

Pia amezema waganga wa tiba asilia wanatakiwa kuepuka matangazo yanayokinzana na sheria, kanuni na taratibu ikiwa pamoja na matangazo ya dawa ambazo hazijafanyiwa uthibitisho kuwa salama.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *