Zaidi ya wafungwa 900 wametoroka baada ya kutokea shambulizi na kuvunja gereza moja nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Watu 11 wameuawa katika tukio hilo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni baada ya kutokea fujo hizo.

Mwanaharakati mmoja anasema kwa makundi mengi yaliyojihami yanayojulikana kama Mai-Mai yanaendesha shughuli zao eneo hilo.

Siku ya Jumamosi wafungwa kadhaa walitoroshwa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha na kuanza kushambulia watu nchini humo.

Mwezi uliopita mamia ya wafungwa walitoroka katika jela moja kubwa mjini Kinshasa baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuvamia jela hiyo usiku wa manane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *