Wafugaji zaidi ya 200 wa kijiji cha Mswaki kilichopo kata ya Masanja wilayani Kilindi Mkoani Tanga wamewazuia watoto wao kwenda shule kwa sababu ya kuhofia usalama wao kutokana na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kati ya wakulima na wafugaji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia wakulima kushambulia kwa mapanga ng’ombe wa wafugaji ambao inadaiwa kuwa waliingia katika shamba la mkulima anayejiandaa na msimu wa kilimo na kusababisha mapigano na ng’ombe 10 kufa na wakulima kujeruhiwa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Ramadhani Sendege amekiri kuwepo hofu ya usalama kwa wanafunzi wanaokwenda shule kwasababu mgogoro wa pande hizo mbili umedumu kwa miaka saba bila kutafutiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Serikali kata ya Masanja, Mary Muhoza amesema kuwa yeye kama mlinzi wa amani atahakikisha analifanyia kazi suala hilo ili wanafunzi waweze kwenda shule bila kuhofia usalama wa maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *