Jeshi la Polisi katika Mji wa Kisumu, nchini Kenya limelazimika kuanza kutumia nguvu kuwatawanya kundi la vijana waliojitokeza mtaani kuanza kuchoma matairi ya magari, wakidai kuibiwa kura kwa mgombea wao wa urais anayeungwa mkono na Muungano wa Nasa, Raila Odinga.

Tukio hilo limetokea baada ya saa chache Odinga kujitokeza mbele ya vyombo vya habari akituhumu uchakachuaji wa kura zake uliofanywa na Tume ya Uchaguzi isiyokuwa na mipaka (IEBC) wakati wa tukio la kuhesabu kura.

Wananchi nchini Kenya walipiga kura katika Uchaguzi Mkuu siku ya jana ,kabla ya vituo hiyo kufungwa kuanzia saa 11:00 jioni.

Polisi walilazimika kutumia nguvu huku wakirusha risasi hewani ili kuwatawanya.

Baadaye Polisi iliamua kuondoa mawe yaliyokuwa yametegwa na vijana hao barabarani.

Katika hatua nyingine, kuna taarifa za kupigana kwa wafuasi wa wagombea ubunge katika kituo vha kujumlishia matokeo , kilichopo Mji wa Mokewe, uliopo Lamu kabla ya Polisi kuwasili eneo la tukio na kurejesha hali ya utulivu

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *