Wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) wamejitokeza katika baadhi ya miji nchini humo kushinikiza kuondolewa kazini kwa baadhi ya maafisa wakuu wa tume ya taifa ya uchaguzi.

Maafisa wa usalama Kenya wamekuwa kishika doria karibu na jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) jijini Nairobi.

Muungano wa Nasa ukiongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano ya kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.

Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika uchaguzi huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *