Waziri wa fedha na mipango nchini, Dr Philip Mpango ameagiza kuondolewa kazini kwa wafanyakazi wanne wa mamlaka ya mapato Tanzani (TRA) katika kituo kidogo cha Forodha cha Manyovu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Burundi baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wao wa kazi.

Waziri huyo aliwasili mkoani humo katika ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo zinazohusu wizara yake.

Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa kwa uongozi wa TRA ni kuhakikisha wafanyakazi wanne wa mamlaka hiyo wanaofanya kazi katika kituo hicho kidogo Forodha cha Manyovu, kilichopo mkoani Kigoma wanaondolewa baada ya kubainika kuwa wanafanya kazi chini ya kiwango na kubainishwa na wafanyabiashara mkoani humo kwamba wanajihusisha na vitendo vya rushwa.

Pia aliwaasa wafanya kazi wa taasisi hiyo kufanya kazi zao kwa uadilifu na kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya serikali na kwamba hawatamuonea huruma mfanyakazi yeyote atakayejihusisa na wizi wa fedha za umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *