Muungano mkubwa wa vyama vya wafanyakazi Afrika kusini (Cosatu) unafanya mgomo wa kitaifa kupinga rushwa.

Kunatarajiwa kuwa na migomo 13 katika miji yote mikuu ikiwemo miji mikubwa kibiashara Johannesburg, Cape Town na Durban.

Katibu mkuu wa muungano wa Cosatu, Jumatano aliwaambia waandishi habari kwamba maandamano hayo yatakuwa makubwa kushinda maandamano mengine yote.

Hatua hiyo inaungwa mkono na mshirika mwingine wa chama tawala ANC, chama cha SACP.

Inaarifiwa pia kwamba waandamanaji watashinikiza kujiuzulu kwa rais Jacob Zuma kutokana na tuhumza hizo za rushwa.

Cosatu imekuwa ikimuunga mkono rais Zuma lakini sasa unamuunga mkono naibu rais Cyril Ramaphosa katika kuwania uongozi dhidi ya Nkosazana Dlamini-Zuma, mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika anayeonekana kupendelewa na rais Zuma kumrithi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *