Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa wamewakamata watu watatu wakijihusisha na biashara ya uuzaji wa shisha katika wilaya ya Kindondoni.

Sirro amesema kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Kinondoni, Suzane Kaganda kuwa wamewakamata watuhumiwa hao wakiwa na vielelezo hivyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwatuhumu kamanda Sirro na kamanda wa Kindondoni, Suzane Kaganda kuwa hawafanya kazi yao ipasavyo kwa kuwaacha wauzaji shisha.

Makonda alisema biashara na uvutaji wa shisha unaendelea licha ya polisi kukanusha kuwapo kwa shughuli hizo katika jiji la Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *