Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera, bunge, kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewaagiza wadaiwa wote wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF, kulipa madeni wanayodaiwa mara moja ili kufankisha mipango ya maendeleo ya shirika hilo.

Ametoa agizo hilo katika ziara yake fupi ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba wa Dungufam unaotekelezwa na NSSF uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo amesema “Tuchukue tu hatua haraka,tena kwa kuzingatia mikataba hiyo hiyo, kwasababu kila mtu alipokuja kukopa alijua mkataba wa ukopaji wake kati yake yeye na NSSF ukoje na unafanyaje na masharti yake yake ya kulipa yako vipi,”.

Pia ameongeza kwa kusema “Ndani ya wiki moja, ninataka kuhakikisha mnachukua hatua haraka sana kushughulika na hao wadaiwa sugu bila kujali ni nani,anafanya nini katika nchi hii ya Tanzania na yuko wapi,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *