Raia wawili wa China Wang Young Jing (37) Chen Chung Bao (35) wamekamatwa na jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa makosa ya utekaji nyara jijini Dar katika eneo la Palm Beach Hotel.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, CP Simon Sirro amesema watu hao walimteka raia wa China mwanamke aitwaye  Liu Hong (48) ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa  Le Grande Cassino waliyemteka Oktoba 23 mwaka huu ambapo  polisi walimkuta akiwa ndani ya chumba cha Hotel ya Palm Beach iliyoko Upanga jijini Dar es Salaam na walimkamata pia mtu aliyekuwa amekodi chumba hicho.

Kamanda Sirro amefafanua kuwa Oktoba 24 majira ya saa kumi na moja jioni kikosi kazi cha wizi wa makosa ya kimtandao cha polisi kilifanikiwa kumtia nguvuni raia mmoja  wa China akiwa ndani ya chumba cha hoteli hiyo baada ya kuvunja mlango.

Sirro amesema baada ya kufungua chumba hicho walimkuta raia aliyetekwa akiwa hajitambui na akiwa na majereha usoni, pia palikutwa vipande vya taulo vyenye damu vilivyotumika kumfungia mikono ambapo alichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Ameeleza kuwa sababu kubwa ya utekaji nyara huo ilikuwa kumtaka majeruhi huyo atoe YEN 100,000 ambazo ni  sawa na dola za Marekani 19,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *