Wachimbaji wadogo  15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ, Nyarugusu mkoani Geita jana wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya hali zao kuendelea vizuri.

Siku ya Jumapili, ilikuwa siku ya muujiza kwa watu hao ambao waliishi chini ya ardhi kwa zaidi ya saa sabini na mbili (72) kabla      ya baadaye kuokolewa katika tukio hilo la kihistoria nchini Tanzania.

geita-3

Januari 25, 2017, watu hao, akiwemo raia mmoja wa China, Meng Juping walifukiwa na kifusi kwenye mgodi huo na hivyo kuishi ardhini kwa muda huo bila kuona jua wala mwanga, hali ambayo kimaumbile ni vigumu kutokana na kukosa hewa safi ya oksijeni ambayo ndiyo humfanya binadamu kuishi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *