Wachezaji wa Yanga wamerejea kufanya mazoezi baada ya jana kugoma kutokana na kutolipwa mishahara yao.

Mazoezi hayo yamefanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa muda wa saa moja leo asubuhi.

Chini ya kocha wa klabu hiyo George Lwandamina, wachezaji hao walifanya mazoezi mapema kabla ya kuondoka na kurejea kwao.

Kabla ya mazoezi wachezaji walifanya kikao cha takribani dakika 17 kabla ya kukubaliana na kufanya mazoezi hayo leo.

Taarifa zilizopo zinasema kuwa wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara yao ila wameahidiwa suala hilo ndani ya siku mbili litakuwa limeisha ila kwasasa wametakiwa waendelee na mazoezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *