Kocha wa Machester United, Jose Mourinho amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo waliwapa mashabiki jezi zao kama zawadi ya sikukuu ya Christmas baada ya mwisho wa mechi dhidi ya West Brom na United kuhinda 2-0.

Akizunguza baada ya mechi hiyo Mourinho amesema kuwa aliwaambia wachezaji wake kutoa jezi hizo kwa mashabiki waliosafiri na timu kama zawadi ya sikukuu ya Christmas.

Mourinho amesema wachezaji nao waliamua kuwapa mashabiki na kama ilivyozoeleka kubadilishana jezi na wachezaji wa timu pinzani lakini wakaamua kuwapa mashaki wao waliokwenda kuwasapoti.

Baada ya mechi hiyo wachezaji wa Manchester United walitoa jezi zao kwa mashabiki wa United waliosafiri na timu hiyo kwa ajili ya kwenda kuisapoti.

Timu hiyo inatarajia kucheza mechi ijayo ya ligi kuu siku ya Boxing Day dhidi ya Sunderland katika uwanja wa Old Trafford ukiwa ni mchezo wa 18 kabla mzunguko wa kwanza kumalizika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *