Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi amewaongoza wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina kususia kuongea na wanahabari baada ya uokosoaji kuhusu uchezaji duni wa timu hiyo.

Messi ametangaza mgomo huo baada ya kufunga bao wakati wa ushindi wao wa 3-0 mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Colombia.

Kituo kimoja cha redio kilikuwa kimeripoti kuwa mshambuliaji Ezequiel Lavezzi alivuta bangi baada ya kipindi cha mazoezi, tuhuma ambazo amekanusha.

Messi na wenzake 25 waliondoka kutoka kwenye kikao na wanahabari bila kuzungumza nao baada ya mechi hiyo dhidi ya Colombia.

Argentina walikosolea sana baada yao kulazwa 3-0 na Brazil lakini ushindi wao dhidi ya Colombia umewawezesha kupaa hadi nambari tano na kwenye nafasi za kushindania kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *