Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule ya awali na Msingi ya Lucky Vincent Academy.

Bunge kwa ujumla limechangia shilingi milioni 100, milioni 86 zimetokana na michango ya wabunge katika kikao cha leo ambapo wameamua posho zao ziende kwa wafiwa hao, huku Bunge lenyewe limetoa milioni 14.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaongoza waombolezaji mbalimbali kuaga miili 35 ya marehemu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Mbali na Makamu wa Rais pia viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuaga miili ya wanafunzi waliofariki kwa ajali Arusha.

Viongozi wengine watakaohudhuria kwenye msiba huo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene na waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndarichako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *