Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, leo kwa mara nyingine wamesusuia kushiriki uapisho wa mbunge mpya wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi CUF, Rehema Juma Migilla aliyeapishwa Bungeni mjini Dodoma leo.

Wabunge hao walikusanyika nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma asubuhi kabla ya Bunge kuanza na muda mfupi baada ya Mbunge huyo Mpya kula kiapo cha Uaminifu Mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai waliingia Bungeni kuendelea na Shughuli za Bunge.

Mgomo wqa Wabunge hao ni muendelezo wa wabunge hao wa kuto kuwapa ushirikiano wabunge wote wapya wa CUF na wale wanaounga mkono upande wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibeahim Lipumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *