Waasi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kiasi cha watu mia moja wameuawa katika maandamano ya kuipinga serikali, katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

Ofisi ya Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila imepinga taarifa hizo, huku ikiwalaaumu viongozi wa maandamano hayo kwa kuchochea ghasia hizo za umwagaji damu.

Waandamanaji nchini Congo.
DRC: Waandamanaji nchini Congo.

Upinzani nchini humo wamevilaumu vyombo vya usalama kwa kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakiandamana kwa amani juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Rais nchini humo.

Wanaamini kuwa Rais Kabila anajaribu kung’ang’ania madaraka hata baada ya kumalizika kwa muhula wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *