Maandamano mapya yametokea katika mji wa St Louis nchini Marekani, ambapo polisi mzungu wa zamani kukutwa hana hatia kwa kumuua mtu mweusi mwaka 2011.

Mamia ya watu waliandaanama katika mji wa Missouri kwa siku ya pili wakisema kuwa maisha ya weusi yana maana.

Zaidi ya waandamanaji 33 walikamatwa na polisi 11 kujeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Ijumaa usiku.

Bwana Stockley na mwenzake walisema waliamini kuwa Bw Smith alikuwa akishriki katika kitendo kinachohusu madawa ya kulevya nje ya mkahawa.

Video ya polisi ilionyesha Bw Smith akirudisha gari nyuma kwenda kwa lile la polisi mara mbili katika jaribio la kutoroka.

Baada ya kumfuata kwa kasi kwa muda wa dakika tatu, Bw Stockley alimuambia mwenzake ambaye alikuwa akiendesha gari aligonge gari la Smith.

Bwa Stockley kisha akakimbia kwenda kwa dirisha la gari la Smith na kumfytulia risasi mara tano.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *