Shrikisho la soka Barani Afrika “CAF” limewateua waamuzi kutoka nchini Algeria kuchezesha pambano la kuhitimisha ratiba kati ya Tanzania na Nigeria ambapo mechi hiyo itachezwa nchini Nigeria.

Waamuzi watakaochezesha pambano hilo ni Mehdi Abid Charef atakayekuwa muamuzi wa kati akisaidiwa na Waalgeria wenzake ambao ni Abdelhak Etchiali na Ahmed Tamen huku mwamuzi wa akiba akiwa Mustapha Ghorbal.

Kamishna wa mchezo huo atakuwa Inyangi Bokinda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo pambano hilo linatarajiwa kuchezwa septemba 3 mwaka huu katika uwanja wa Adokiye Amiesiamaka katika mji wa Port Harcourt  nchini Nigeria.

Mechi ya kwanza kati ya timu hizo ilifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo zilitoka 0-0.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *