Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imeahirisha kesi inayomkabili mfanyabiashaa Mohamed Mustapha na mwenzake Samwel Lema wanaodaiwa kuiibia serikali shilingi milioni saba kwa kila dakika, kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena Agosti 18 mwaka huu huku watuhumiwa wamerudishwa rumande.

Hakimu aliyekuwa akisoma shauri la kesi hiyo, Wilbard Mashauri amesema watuhumiwa hawawezi kupewa dhamana na mahakama hiyo kwa kuwa haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa watuhumiwa wa kesi hiyo

Wafanyabiashara Mohamed Yusufali na mwenzake Samwel Lema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Engineering Works Limited wakikabiliwa na mashitaka 222 ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 14.

Washtakiwa wanadaiwa kujipatia pesa hizo kwa njia ya udanganyifu katika mapato ya serikali, Samwel Lema ambaye anadaiwa kusababisha hasara kwa kughushi na kukwepa kulipa kodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *