Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kuvifanyia uhakiki vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuanzia kesho.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu, zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Tarishi amesema katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo, vyuo vyote pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), leo vitatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU.

Amesisitiza kuwa mwanafunzi yeyote ambaye hatazingatia maagizo hayo ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametangaza kuanzisha msako wa wanafunzi hewa vyuoni baada ya kubainika kuwepo kwa wanafunzi hewa wanaopewa mikopo wakiwemo wengine wanaosoma shahada huku wakiwa hawana sifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *