Mashirika matano ya utangazaji nchini Marekani yamezuiliwa kuhudhuria mkutano wa wanahabari katika viwanja vya Ikulu ya Rais wa Marekani ya White House kilichofanyika jana.

Mashirikia yaliyozuiliwa kuhudhuriwa kwenye mkutano huo ni CNN, The New York Times,Politico, Los Angeles Times na BuzzFeed ambapo mkutano huo uliitishwa na msemaji wa Ikulu ya Rais wa Marekani, Sean Spicer.

Spicer hakutoa maelezo kwanini waandishi wa habari wa mashirika hayo waliachwa nje ya kikao kisicho rasmi cha wanahabari, hatua ambayo imeibua shutuma kalinchini.

Shirika la habari la Reuters pamoja na mashirika mengine 10 yakiwemo Bloomberg na CBS yaliruhusiwa kuhudhuria mkutano huo wa wanahabari.

Wakati wanahabari kutoka CNN na mashirika mengine yaliyoathiriwa yalipojaribu kuingia IKulu, yalizuiwa kwa kuambiwa majina yao hayako katika orodha ya wanahabari walioalikwa.

Utawala wa Rais Donald Trump umekuwa ukiyashutumu mashirika hayo kuwa yanaeneza habari za uongo na za kupotosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *