Vyombo vya habari nchini Uganda vimepigwa marufuku kufanya mahojiano na mwanamuziki wa nchi hiyo Bobi Wine.

Marufuku hayo yametolewa na Tume ya mawasiliano nchini humo (UCC) kutokana na mwanamuziki huyo kuwa kinara kwenye suala la kupinga ukomo wa urais nchini humo.

Bobi Wine ambaye ni mbunge wa upinzani ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuhusu suala hilo.

Bobi Wine amesema kuwa amepigiwa simu na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na kuthibitisha suala hilo, kuwa wamepigwa marufuku kufanya naye mahojiano yoyote.

Ameandika “Hii asubuhi nilitakiwa kufanya mahojiano na Capital FM, baadaye nikataarifiwa kuwa wamepewa agizo na UCC na kupigiwa simu na watu wa usalama kwamba wasiwe na mimi, nikapigiwa simu na vituo vingine vya redio na runinga na kunithibitishia wamepewa agizo hilo hilo na kwa vitisho, na iwapo watakuwa na mimi watakuwa katika hatari ya kufungiwa”,.

Bobi WIne amekuwa miongoni mwa viongozi maarufu ambao wanapinga vikali suala la kutaka kupitishwa kwa katiba ambayo itongeza muda wa ukomo wa urais, kitendo ambacho kitamruhusu Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo, kugombea tena awamu ijayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *