Mechi za ligi kuu Tanzania Bara zinaendelea tena leo kwa michezo sita katika viwanja tofauti nchini.

Simba SC watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati Yanga itamenyana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Africans Lyon itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji.

Ndanda itacheza dhidi ya Tanzanai Prisons kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ligi hiyo itaendelea Alhamisi Novemba 3, mwaka huu kwa michezo miwili ambayo itafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Mwadui kuialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex huko Shinyanga huku Mbao Fc ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *