Staa wa Bongo fleva, Voice Wonder amabaye alipata umaarufu kupitia wimbo wake ulioitwa  ‘Nimpende Nani’ amesama kwamba anajipanga kurudi tena kwenye game na kuvunja ukimya wake wa muda mrefu bila kutoa ngoma.

Voice Wonder amesema kuwa hakuna anayeweza kubisha kuwa muziki wa Tanzania umetawaliwa na wasanii wawili tu, akimaanisha Diamond na Alikiba na kudai kuwa wengi wameshindwa kufikia ukubwa huo.

Staa huyo pia amedai alichojifunza kwenye muziki wa sasa ni kuwa idea za nyimbo nyingi zinafanana kuanzia mashairi na melody hivyo hakuna kinachomshtua kwasasa kama akihamua kurudi katika uimbaji.

Vile vile Voice Wonder amedai kuwa tayari ana ngoma tatu ambazo amesharekodi ambazo amewashirikisha mastaa wengine wa muziki huo ambao ni Christian Bella, Q-Chief na Madee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *