Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, imeomba viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi, watoe msaada wa kuzalisha vifaa maalum vyenye nembo Kagera na bei ndogo ili kuwezeshe waathirika wa tetemeko la ardhi Bukoba, waweze kujenga nyumba zao kwa haraka.

Hayo yamesemwa Mkurugenzi Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bregedia Jenerali Mbazi Msuya katika mafunzo ya siku mbili ya wanahabari, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za Kiraia ya kuwajengea uwezo Masuala ya Maafa na kutaka vifaa hivyo kuzalishwa katika kipindi cha miaka miwili.

Brigedia Msuya amewataka wazalishaji hao kutumia fursa hiyo itakapopata kibali na kuwa bati pamoja na mfuko wa Saruji, viuzwe kwaajili ya kuchangia wahanga wa tetemeko wa Kagera kutokan na kuongezeka kwa mahitaji makubwa ya vifaa hivyo kwa sasa.

Aidha ameongeza kuwa kamati ya Maafa ya Mkoa huo kwa kushirikiana na Idara ya Maafa, wameamua kuwapa wahanga wa tetemeko kila familia bati 20, mifuko mitano ya Saruji, Blanketi moja kwa kila mtu hata kama mtoto na mkeka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *