Chama cha wachapishaji binafsi nchini Tanzania (PATA) kimeiomba Serikali kuviondoa mara moja shuleni vitabu vyote vilivyoandaliwa na kuchapishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mara baada ya kubainika kutokidhi vigezo na kuwa na mapungufu.

Gabriel Kitua ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho amesema vitabu hivyo havikupitia mchakato na kufuata mwongozo wa Wizara ya elimu na ikiwa vitaachwa mashuleni vitaleta athari kubwa katika ustawi wa elimu nchini.

Kitua amesema makosa mengi yaliyobainika yapo kwenye vitabu vya Hisabati kidato cha tano na kidato cha sita,historia kidato cha tatu na vitabu vyote vya kingereza kwa darasa la tatu na kidato cha kwanza hadi nne.

Sakata la kuwepo kwa vitabu vyenye mapungufu shuleni liliibuliwa bungeni mjini Dodoma huku tayari vikiwa mashuleni kwa ajili ya kufundishia wanafunzi mashuleni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *