Klabu ya Real Madrid itacheza dhidi ya mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Real Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano ya Ulaya, walifanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuwavurumisha Juventus FC ya Italia jumla ya mabao manne kwa matatu.

FC Bayern Munich, nao waliwafungashia virago Valencia CF ya Hispania hatua ya robo fainali kwa kuwafumnga jumla ya mabao 2-1.

 Mchezo mwingine wa nusu fainali utakua kati ya majogoo wa jiji (Liverpool FC) kutoka England wamepangwa kukutana na AS Roma ya Italia.

Liverpool walifanikiwa kuitoa Man City katika mchezo wa robo fainali kwa jumla ya mabao matano kwa moja, ili hali AS Roma waliitupa nje FC Barcelona kwa jumla ya mabao manne kwa matatu.

 

Liverpool itaanzia nyumbani dhidi ya AS Roma huku Real Madrid ikiwa ugenini kuikabili Bayern Munich.

 

Mechi za kwanza zitapigwa kati ya tarehe 24/25 Aprili 2018 huku za marudiano zikichezwa kati ya tarehe 1/2 May 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *